Shalom mtumishi wa Bwana, nina chukua nafasi hii kukukaribisha kusikilliza Jerusalem Online Radio! hii ni radio inayokuletea Neno la Mugnu, mafundisho ya Kiroho, na nyimbo za injili zenye kubariki na kujenga imani yako. Lengo letu kuu ni kuhakikisha kuwa Injili inawafikia watu wote popote walipo duniani kupitia mtandao wa internet. Ungana nasi kila siku upate yale ambayo Mungu amekuthudia kwa ajili ya maisha yako, hizi ni siku za mwisho ambapo watu wengi kwa sasa wamepotoshwa na maneno ya uovu, lakini Mungu ameachilia Neema kwa ajili ya Neno la Kweli itakayo tusaidia kuijuwa kweli ya Mungu. Ahsante kwa kuwa nasi kama familia ya watakatifu waendao Mbinguni na kuwa sehemu ya familia ya Jerusalem Online Radio. Mungu akubariki sana. Amen!